The House of Favourite Newspapers

VERA SIDIKA AIBUA JAMAA MPYA!

Vera Sidika

ZIKIWA zimepita wiki kadhaa tangu drama ya muuza nyago maarufu nchini Kenya, Vera Sidika kudaiwa kutemana na bwana’ke ambaye pia ni mwanamuziki nchini humo, Otile Brown, mwanadada huyo ameibuka na jamaa mpya.

Juzikati picha za kumwaga zilivuja zikimuonesha mwanadada huyo akiwa na jamaa huyo mpya usiku wakijiachia na kupata msosi wa maana.

Vera na Otile walimwagana huku chanzo kikieleza kuwa kila mmoja alikuwa akinufaika kwa upande wake. Inaelezwa kuwa, Vera alikuwa akimtumia Otile kutengeneza jina lake kuendelea kuwa juu wakati Otile alikuwa akimtumia kufanikisha muziki wake akimtumia kama video queen.

Comments are closed.