The House of Favourite Newspapers

Viboko wa Pablo Escobar Kutambuliwa Kisheria Kama Watu

0

Mahakama ya nchini Marekani imepitisha sheria ya kuwatambua Viboko waliokuwa wanamilikiwa na muuzaji hatari wa madawa ya kulevya nchini Kolombia, Pablo Escobar kama watu, kufuatia kesi dhidi ya Serikali ya nchi ya Kolombia juu ya kuwauwa na kuwafanya viboko hawo wawe tasa ili wasiweze kuzaliana zaidi nchini humo.

 

Viboko hao walipelekwa nchini Kolombia mwaka 1980 na Pablo Escobar ambaye alifariki mwaka 1993 , tangu hapo viboko hao hawakuwa na muangalizi hivyo kuzagaa ovyo na kuzaliana bila uangalizi. Ripoti zinasema kwa miaka nane viboko hao wameongezeka kutoka 35 hadi 80.

 

Makundi ya wanasayansi nchini Kolombia yametahadharisha hatari ya viboko hao kwa binadamu, sheria iliyopitishwa nchini Marekani juu ya kuwatambuwa Viboko kama binadamu inaweza isichukuliwe kwa uzito nchini Kolombia.

Cc; @bakarimahundu

Leave A Reply