The House of Favourite Newspapers

Gwajima Atangaza Kugombea Ubunge Kawe

0

ASKOFU Josephat Gwajima ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo jana,  Julai 1, 2020,  alifika kwenye ofisi za chama hicho kupewa taratibu za mchakato huo.

 

Kuhusu kuunga mkono umoja wa vyama vya upinzani (Ukawa) mwaka 2015, amesema hajawahi kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema) ila hulka yake ni kutetea haki ilipo wakati wote.

 

Amesema alikwenda Ofisi ya CCM Wilaya ya Kinondoni baada ya kumsikia Rais John Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM, Ally Bashiru, akitangaza kuwa wale wenye nia ya kumsaidia rais wachukue fomu, hivyo  na  ndiyo maana alifika kwenye ofisi hiyo kujua utaratibu unaotakiwa.

Amesema kuwa mtu mchungaji hakumzuii kuwa mbunge kwa kuwa wako viongozi wa dini ambao pia ni viongozi wa kisiasa kwani alikuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 1994.

 

Askofu huyo hakusema kitu ambacho atawafanyia watu wa Kawe iwapo atapata nafasi hiyo.   Pia alisema ilionekana kuwa angeweza kugombea huko Misungwi, lakini, kwa mujibu wake, Misungwi ni sehemu aliyozaliwa lakini maisha yake yamekuwa Kawe kwa hiyo atagombea Kawe.

 

Leave A Reply