The House of Favourite Newspapers

Video: Koffi alivyompiga Dansa wake wa kike baada ya kutua Nairobi

0

KOFFI (1)Koffi Olomide akimpiga mateke mnenguaji wake.

JANA Ijumaa Standard Media Digital ya Kenya ilitoa video ikionyesha Staa wa Muziki wa Kongo, Koffi Olomide akimpiga mateke dancer wake wa kike muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege,  Jomo Kenyatta International Airport kwa ajili ya kufanya shoo.

KOFFI (2)Bila kueleza sababu, lakini video hiyo inaonyesha kulikuwa na drama inaendelea, Koffi akiwa mwenye hasira alimfuata dada huyo na kumpiga teke hadharani. Cha kushangaza polisi pia wanaonekana kwenye video hiyo lakini hakuna aliyethubutu kuchukua hatua yoyote.

Watu wanajiuliza, kama anaweza kumpiga mwanamke mbela ya kamera hivi, je inakuwaje wakiwa huko mafichoni. Wakenya wengi wamekuja juu kwenye mitandao, wanadai huyu jamaa ni women abuser, hivyo kuna hashtag inaendelea kwenye Facebook na Twittwer sasa ‪#‎KenyansboycottKoffiOlomide‬

Angalia video hapa:

Leave A Reply