The House of Favourite Newspapers

VIDEO: MAMBOSASA Ataja Sababu za Kumkamata Mwandishi

KAMANDA wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa,   leo Jumanne Julai 30, 2019, amezungumza na waandishi wa habari na amesema walimkamata mwandishi wa habari, Erick Kabendera, Jumatatu, Julai 29, 2019,  baada ya kupelekewa wito wa kufika polisi lakini akakaidi na bado wanaendelea kumshikilia kwa mahojiano kuhusu uraia wake.

“Mwandishi huyo aliandikiwa barua ya wito kwa ajili ya mahojiano lakini alikaidi kutii wito huo.  Kila mmoja anapaswa kutii wito bila shuruti na kila mmoja anapaswa kutii ili kuondoa msuguano usiokuwa na lazima.  Polisi tunapomwita kwa hiari akakaid;  tunatumia mamlaka tuliyopewa kisheria,” amesema Mambosasa na kuongeza:

“Baada ya kukamatwa, tumesikia taarifa mbalimbali na waandishi wa habari wengine wakisema ametekwa.  Niseme kuwa mwandishi huyo hakutekwa, aliitwa lakini kwa ujeuri akawa amekaidi wito huo.

“Tunaendelea kuwasiliana na maofisa uhamiaji ili lile alilotuhumiwa nalo linawekwa mezani kwa yeye kuwahakikishia hao wanaohoji Utanzania wake, na ni rahisi kuthibitisha hilo. Lakini kwa kuwa yeye mwenyewe ana mashaka, akakataa kutii sasa tunaye na taratibu zingine zinafuata.”

Comments are closed.