The House of Favourite Newspapers

Amberr Washington Aifagilia Global Group (Picha +Video)

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akiongea  na Makamu wa Rais wa Tuzo za Hollywood and African Prestigious (HAPA), Amberr Washington,  ofisini kwake alipotembelea makao makuu ya Global Group yaliyoko Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam.

MAKAMU wa Rais wa Tuzo za Hollywood and African Prestigious (HAPA) kutoka Marekani, Amberr Washington, ametua ndani ya mjengo wa Global Group, Sinza-Mori jijini Dar na kueleza namna walivyojipanga kutoa fursa kwa vijana wenye vipaji mbalimbali nchini Tanzania.

Amber amewapongeza wafanyakazi wa Global Group kwa namna walivyompokea na jinsi wanavyofanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu.

Mmarekani huyo mwenye asili ya Afrika,  alikuwa ameongozana na Balozi wa Tuzo hizo nchini ambaye pia ni mmiliki wa Master Tanzania, Mawini Casy,  na mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda,  Ofisa Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Henry Mrutu na ofisa Sanaa Mwandamizi wa Basata, Godffrey Nago.

Abdallah Mrisho  akiwa na Amberr Washington na Balozi wa HAPA nchini Tanzania, Mawini Casy.
Amberr  akikabidhiwa Gazeti la Ijuma Wikienda na Mhariri wa Gazeti hilo, Sifael Paul. Wa pili kulia ni Meneja wa +255 Global Radio, Bori Mbaraka na  kulia ni Mawini Casy ambapo  Mhariri wa Global TV, Nyalobi Kelvin. anaonekana kwa nyuma.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo (katikati) akiwa na Amberr  baada ya kufika ofisini kwake. Wa pili kulia ni Ofisa Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Henry Mrutu,akifuatiwa na Mawini Casy, na kushoto ni Ofisa Sanaa Mwandamizi wa Basata, Godfrey Nago.
Mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda akiwa na Amberr walipofika ofisi za Global Group.

Comments are closed.