The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mwakinyo Atamba Hajaona Wa Kupigana Naye Nchini


Bondia Hassan Mwakinyo (kulia) akisalimiana na Meneja wa Global Group Abdallah Mrisho ofisini, Sinza Mori, Dar

 

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo, amesema kuwa hajaona bondia wa kupigana naye hapa nchini na jeuri hiyo anaipata kutokana na udhamini anaoupata kutoka Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Michezo, SportPesa.

Bondia Hassan Mwakinyo (Kulia) akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, leo Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori, Dar.

Kauli hiyo, aliitoa  Jumanne ya Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea ofisi za Global Group inayochapisha magazeti ya  Championi, Spoti Xtra, Uwazi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi Mchanganyiko, pamoja na vituo vya mtandaoni vya Global TV Online na +255 Global Radio,  Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

Bondia Hassan Mwakinyo akifafanua jambo kitaalamu kwa Mhariri Mtendaji wa Global Group Saleh Ally.

Mwakinyo, wikiendi iliyopita alifanikiwa kumpiga mpinzani wake Muargentina, Sergio Gonzalez kwa KO katika raundi ya tano ya pambano hilo lililopigwa nchini Kenya.

 

Akizungumza mara baada ya kutembelea kampuni hiyo, Mwakinyo alisema kuwa malengo yake hivi sasa yanafikiria kupigana mapambano ya kimataifa na siyo kitaifa kutokana na kutomuona bondia mwenye uwezo wa kupigana naye.

Bondia, Hassan Mwakinyo (aliyekunja ngumi) akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa gazeti la Championi.

Mwakinyo alisema, kwa kupitia SportPesa hivi sasa ana uhakika wa kufanya mazoezi mara mbili kwa siku huku akiwa na uhakika wa kula chakula safi. Ana udhamini wa miaka mitatu wa SportPesa.

 

“Binafsi sijaona bondia yeyote wa kupigana na mimi kwa bondia wa hapa nchini na hilo lipo wazi kutokana na kiwango changu nilichonacho hivi sasa.

Hassan Mwakinyo (aliyevaa kofia) akiwa kwenye picha ya pamoja na team ya 255 Global Radio Sinza Mori, Dar.

“Nafahamu hivi sasa kila bondia anataka kupigana na mimi, lakini niwaambie kwangu sijamuona, kama yupo basi hamna shida ajiandae na uwekwe mkwanja wa kutosha utakaonishawishi kupigana.

BONDIA Hassan Mwakinyo akifafanua jambo wakati akifanyiwa mahojiano kwenye 255 Global Radio iliyopo Sinza-Mori, Dar.

“Nitakuwa tayari kupigana popote pale atakapotaka mpinzani wangu, hata kama ni sebuleni kwake,” alisema Mwakinyo.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

Comments are closed.