The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mwili wa GODZILLA Waagwa SALASALA, Kuzikwa Kinondoni

BAADA ya kifo cha ghafl a cha Msanii wa Muziki wa HipHop Bongo, Golden Mbunda ‘Godzilla’, kuleta mshituko mkubwa, leo Jumamosi saa 7 mchana anatarajiwa kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Enzi za uhai wake, Godzilla aliwahi kutikisa tasnia hiyo kwa ngoma kali kama vile, Nataka Mkwanja, First Class aliyomshirikisha Mwasiti, Thanks God aliyomshirikisha Walter Chilambo, Stay, Nataka, KingZilla, Get High na Lakuchumpa.

Akizunguza mapema jana, msemaji wa familia hiyo baba mkubwa wa marehemu, Shida Msolwa, alisema mazishi ya mpendwa wao huyo yatafanyika leo saa 7 mchana kwenye Makaburi ya Kinondoni jiji Dar es Salaam.

 

Kabla ya taarifa hizi za maziko kutajwa, juzi dada wa marehemu, Joyce Mbunda, alisema marehemu Godzilla alifariki baada ya kushukwa na  presha iliyosababishwa na tatizo la kisukari mwilini.

Alisema, mdogo wake hajaugua kwa muda mrefu, isipokuwa usiku wa kuamkia Jamatatu baada ya kutoka matembezini alipitiliza chumbani kwake kulala ambapo alilala kwa muda mrefu tofauti na ilivyozoeleka, na alipoamka aliomba apewe barafu kwa madai alikuwa akijisikia vibaya. Baada ya kumpatia barafu hiyo na kunywa ghafl a alianza kutapika mfululizo ndipo wakaamua kumpeleka kwenye Zahanati ya Mico iliyopo maeneo ya Salasala na kufanyiwa vipimo ambapo aligundulika presha imeshuka na matatizo ya kisukari.

“Baada ya daktari kuona hivyo aliamua kumpa kitanda kisha akamtundikia dripu lakini kama baada ya saa moja mbele akasema anajisikia vizuri ndipo daktari wa zahanati hiyo akaturuhusu tumrudishe nyumbani, lakini baada tu ya kufi ka nyumbani, muda kidogo alianza kujisikia vibaya tena.

“Mimi nilimshikilia maana alikuwa anang’ang’ana atoke nje, lakini tukambembeleza akatulia, nikamuacha na mama, mimi nikaomba kwenda kulala, muda kidogo tu, Godzilla alikuja chumbani kwangu akisema nisogee tulale pamoja kwa kuwa alikuwa anasikia watu wanamuita nje, hivyo akawa anaomba nimchunge. “Akiwa katika hali hiyo, ghafl a tena alionekana kusimama na kutaka kukimbia nje ndipo nikamshikilia na baadaye mama akaja baada ya muda tukamuomba akae, alipokaa tu akanifi a mikononi, ndiyo tukampeleka Hospitali ya Lugalo,” alisema Joyce.

Comments are closed.