The House of Favourite Newspapers

Video: Rais Samia Amuapisha Makonda Na Viongozi Wengine Aliowateua Ikulu, Dar

0
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Deogratius John Pancras Ndejembi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Rais Samia akimuapisha Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Rais Samia akimuapisha Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa mkoa wa Mara.
Rais Samia akimuapisha Mhandisi Kundo Andrea Mathew kuwa Naibu Waziri wa Maji.
Rais Samia akimuapisha Maryprisca Winfred Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Rais Samia akimuapisha Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Rais Samia akimuapisha Eva Kiaki Nkya kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.
Viongozi mbalimbali Wakiapa Kiapo cha Maadili kwa viongozi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Rais Samia akimuapisha Sylvester Joseph Kainda kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Rais Samia akimuapisha Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Rais Samia akimuapisha Zainab Athuman Katimba kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Rais Samia akimuapisha Daniel Baran Sillo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha Viongozi Wateule katika ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 04 Aprili, 2024

Leave A Reply