The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Wabunge Waonesha ‘Mahaba’ Yao Baada Rais Kikwete Kuibuka Bungeni

DODOMA: Wabunge wa Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania leo Aprili 4, 2017 wameonyesha upendo wao wa dhati ‘mahaba’ kwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipoibuka Bungeni Kushuhudia kuapishwa kwa mkewe, Mama Salma Kikwete aliyeteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni kuwa Mbunge.

Wabunge hao hawakutaka kuficha hisia zao kuonesha kuwa wamemmiss Mzee Kikwete walianza kumshangilia kwa nguvu mara baada ya Spika Job Ndugai kutambulisha ugeni wake, huku wengine wakichombeza kuwa wamemkumbuka Kikwete na wangetamani ashuke kutoka viti vya juu (ambako huketi wageni) ili akasalimiane na Spika.

Akiwa bungeni, Rais Kikwete alisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Viti Maalum-CHADEMA, marehemu Dkt. Elly Macha.

TAZAMA LIVE WABUNGE WALIVYOMSHANGILIA JK

Comments are closed.