The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mara Baada ya Kuapishwa, Hili Ndilo lilikuwa Swali la Kwanza la Mama Salma Kikwete Bungeni


Aliyekuwa mbunge mteule, Salma Rashid Kikwete amekula kiapo leo asubuhi katika mkutano wa saba wa Bunge la bajeti na kuwa mbunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kwa mijibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Machi 1 mwaka huu, ilieleza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Salma Kikwete ameapishwa leo kabla ya shughuli za Bunge kuendelea ambapo miongoni mwa waliohudhuria tukio hilo la kuwapishwa ni mumewe, Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma Kikwete na mtoto wao, Ally Kikwete walivyokuwa Bungeni leo.

Baada ya kuapa, Salma Kikwete amepata nafasi ya kuuliza swali lake la kwanza kama mbunge na alilielekeza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo alitaka kujua, ni upi mpango madhubuti wa serikali katika kutumia fedha za TASAF kusaidia watu maskini mkoani Lindi?

Aidha, Waziri Kairuki alijibu kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inatumia fedha hizo kusaidia kutokomeza umasikini nchini kote kwani inatambua kuwa, umasikini ni kikwazo kikubwa katika kujikwamua kiuchumi.

TAZAMA KILICHOJIRI BUNGENI LEO

Comments are closed.