Video: ‘Wachawi Walinigeuza Fisi Nibebe Maiti – Nimeteseka Zaidi Ya Miaka 14’ – Mtumishi Mathayo Darema

Katika kijiji cha Balangda, wilayani Hanang’, mkoani Manyara, anaishi Mathayo Darema, mtumishi wa Mungu mwenye ulemavu ambaye miaka mitatu iliyopita alifunga ndoa iliyoibua mijadala na maswali mengi katika jamii. Licha ya mashaka hayo, leo ndoa yake inaendelea kuwa imara, na familia hiyo imebarikiwa kupata watoto watatu.
Safari ya maisha ya Mathayo si ya kawaida. Kupitia mahojiano maalum aliyoyafanya na mwandishi wa Global TV, @hoseaelnino, Mathayo anaeleza kuwa ndoa yake ni sehemu ya ushuhuda mpana wa maisha aliyopitia maisha yaliyojaa changamoto, maumivu na majaribu yaliyodhaniwa yangemvunja moyo, lakini hatimaye yakamjenga.
Akizungumza katika mahojiano hayo, Mathayo anaeleza kuwa kabla ya kufunga ndoa, maisha yake yaligubikwa na misukosuko mizito, ambapo kwa zaidi ya miaka 14 alipitia mateso makubwa yanayohusishwa na nguvu za giza, hali ambayo ilihatarisha maisha yake.
Video full ipo YouTube ya Global TV
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

