The House of Favourite Newspapers

VIGOGO WALIOTELEKEZA WATOTO WAFIKIA 107, MSAKO KUANZA KESHO

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akizungumza na baadhi ya wanawake waliojitokeza kupeleka malalamiko yao kwake.
Baadhi ya wanawake waliojitokeza kupeleka malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakimsikiliza kwa makini. 

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa kuanzia kesho Alhamis wanaume wote ambao tayari wametajwa kutelekeza watoto wataanza kupelekewa barua za wito.

 

Akizungumza na baadhi ya wanawake waliojitokeza kupeleka malalamiko yao, Makonda, amesema kuwa hakutakuwa na kigogo yoyote atakayehitaji kuonana naye kwa siri kama ambavyo wengi wamekuwa wakiomba kufanya hivyo na kueleza kuwa nafasi hiyo haipo.

 

Amesema kuwa vigogo 107 tayari wametajwa kutelekeza watoto na amewaomba mara wapatapo wito wa barua yake wafike ofisini kwake mara moja kwani watakaokaidi watachukuliwa hatua kali za kesheria.

 

 Mbali na zoezi hilo Makonda amesema kuwa wadau mbalimbali wamejitokeza kusaidia kuwalipia watoto hao Bima za afya ili waweze kumudu gharama za matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

 

Na Denis Mtima/Gpl.

 

Comments are closed.