Chuchu: Wanaoendekeza Za Utupu Watajuta!

Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans.

STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans amewananga wauza nyago ambao wameibuka na picha za utupu kwa lengo la kusaka umaarufu na kusema kuwa, kitendo hicho madhara yake ni makubwa siku zijazo kwani wanaweza kukosa waume wa kuwaoa.

 

Akipiga stori na paparazi wetu, Chuchu ambaye amejituliza na kuzaa na muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’, alisema amekuwa akiona wasanii wengi wanaoibuka sasa kwenye sanaa hususan wanaojihusisha na umodo katika video za muziki, wakisambaza picha zao za utupu kwa lengo la kupata umaarufu bila kujua wanajiharibia.

 

“Niwatahadharishe tu wasanii wenzangu waachane na haya mambo, wengine hata nguo hawavai kisa kusaka umaarufu. Mwanamke ukiwa hivyo ukija kushtuka baadae utajikuta umeshajiharibia kila kona, hata mwanaume wa maana wa kutulia naye huwezi kupata, mimi nilipata umaarufu kwa filamu ya Roho Sita, sikuvaa nusu utupu,”alisema Chuchu.

Stori: Mayasa Mariwata

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment