The House of Favourite Newspapers

Viongozi wa upinzani Senegal waachiwa huru siku chache kabla ya uchaguzi

0

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko na mgombea urais anayemuunga mkono katika uchaguzi uliocheleweshwa mwezi huu,Bassirou Diomaye Faye, wameachiwa huru kutoka gerezani.

Wawili hao walikutana na mamia ya wafuasi wao waliokuwa na furaha katika mji mkuu, Dakar, baada ya kuachiwa siku ya Alhamisi.

Kuachiwa kwao kulifuatia msamaha uliotangazwa na Rais Macky Sall.

Uchaguzi huo unatazamiwa kufanyika tarehe 24 Machi baada ya kushindwa kwa jitihada za kuuahirisha hadi Desemba.

“Ni siku nzuri zaidi maishani mwangu,” mfuasi mmoja aliambia BBC.

Bw Faye, 44, ni mmoja wa wagombea 19 wanaoshiriki uchaguzi huo.

Anawania kupitia chama cha muungano cha Rais wa Diomaye.

Yacine Fall, makamu wa rais wa chama kilichovunjwa cha Bw Sonko cha Pastef ambacho sasa kinamuunga mkono Bw Faye, alisema: “Tumefurahishwa sana na kuachiwa kwao”.

VANESSA ACHINJWA na KIJANA ALIYEMKATAA KIMAPENZI – MAMA ASIMULIA MWILI ALIVYOUKUTA CHUMBANI…

Leave A Reply