The House of Favourite Newspapers

Viongozi Waungana na Kikwete Mazishi ya Baba Mkwe Wake – Video

MWILI wa mzee Rashid Mkwachu ambaye alikuwa Baba Mkwe wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rashid aliyefariki dunia jana Alhamisi umezikwa leo Ijumaa, Julai 20, 2018 katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Viongozi mbalimbali waandamizi na wastaafu wamejitokeza katika kumsindikiza Mzee Mkwachu ambaye ni Baba Mzazi wa Mke wa Kikwete, Mama Salma Kikwete.

Baadhi ya viongozi hao ni Mkwe wa Marehemu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, mjukuu wa Marehemu ambaye pia ni Mbunge wa chalinze, Ridhiwani Kikwete, Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassani Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Mizengo Pinda, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar mstaafu, Said Meck Sadick, Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Davis Mwamnyange, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma , Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar mstaafu, Suleimani Kova, Wabunge, Freeman Mbowe, Zitto Kabwe.

Viongozi wengine wa dini ni Mufti wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi Bin Ally, Shehe Mkuu wa Dar, Sheikh Alhadi Mussa na wengine.

     

Picha na Richard Bukos | Gpl

FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.