The House of Favourite Newspapers

Vita ya Azam FC na Lipuli haisimuliki

AISEEE! leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi kutakuwa na mchezo usiosimulika kwa timu za Lipuli FC kuvaana na Azam FC kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) na bingwa ataenda Caf.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa Lipuli ya Iringa kucheza fainali ya FA wakati Azam FC ni mara ya pili na bingwa atakwenda kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Azam ilitinga fainali baada ya kuichapa KMC bao 1-0 wakati Lipuli iliiondosha Yanga kwa mabao 2-0.

Kocha wa Azam FC, Idd Cheche ameliambia Championi Jumamosi kuwa, ni mchezo wao wa mwisho msimu huu wa mashidano hivyo lazima watumie nguvu kubwa kuupata ubingwa utakaowarudisha kwenye anga za kimataifa.

 

“Hatujashiriki michuano ya kimataifa kwa muda mrefu na malengo yetu kwa msimu huu ilikuwa ni kushiriki michuano ya kimataifa hivyo kwa kukosa kombe la ligi tunaibukia kwa kutumia Kombe la Shirikisho,” alisema Cheche.

Naye Kocha wa Lipuli FC, Selemani Matola alisema kuwa, licha ya kubanwa na ratiba ni lazima atapapambana kuhakikisha anapata matokeo mazuri.

 

“Kiukweli timu yangu inapitia maumivu makubwa kuanzia ratiba mpaka uwanja kutokuwa rafiki, yote tunaachana nayo tutapambana kupata ushindi, hivyo mashabiki wajitokeze kutupa sapoti,” alisema Matola.
Lunyamadzo

Comments are closed.