The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yazindua Msimu Mpya wa Tusua Mapene, Magari Manne Mapya Kutolewa

0
Moja ya gari zinazoshindaniwa.

 

 

DAR ES SALAAM. Vodacom Tanzania leo imezindua msimu mpya wa shindano lake la ‘Tusua Mapene’ kwa kipindi kitakachoishia tarehe 30, Juni 2022 ambapo washindi watatu watajinyakulia magari mapya huku mshindi wa jumla akijishindia pesa taslimu hadi shilingi milioni 300.

Bw. Nguvu Kamando Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za Ziada (Digital & VAS) akizungumza kwenye uzinduzi huo.

 

 

Mchezo wa ‘Tusua Mapene’ msimu uliopita ulianza rasmi mwezi wa saba mwaka jana na uko wazi kwa wateja wa Vodacom wenye umri wa miaka 18 na zaidi na unawapa wachezaji wote nafasi sawa ya kushinda zawadi kadhaa na pesa taslimu kila siku, kila mwezi na zawadi kuu ya mwisho.

Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisa nchini, Rasul Masudi akizungumza kwenye uzinduzi huo.

 

 

Akizungumzia uzinduzi wa shindano hilo jipya Bw. Nguvu Kamando Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za Ziada (Digital & VAS) alisema ;

 

Uzinduzi rasmi ukifanyika kwa ishara ya funguo kuashiria utoaji wa zawadi ya gari hizo.

 

 

“Vodacom Tanzania tunajivunia kuwa wasikivu kwa mahitaji ya wateja wetu. Kutokana na mabadiliko makubwa na chanya waliyopata washindi wa misimu iliyopita ya ‘Tusua Mapene’ Vodacom imeona itakuwa vyema kuongeza msimu mwingine ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengi zaidi kujishindia zawadi hizo na kutimiza ndoto zao”.

Nguvu Kamando Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za Ziada (Digital & VAS) akikata utepe kuashiria uzinduzi huo.

 

 

“Tusua Mapene inatoa nafasi kwa wachezaji kushinda zawadi moja ya papo kwa papo ya shilingi milioni 100, zawadi nyingi 20 za shilingi milioni 10 na washindi wengine 100 wanaweza kushinda shilingi milioni moja.

Madansa wakinogesha uzinduzi huo.

 

 

“Vilevile kuna zawadi za kila siku kuanzia laki 5 hadi milioni 20 na kutakuwa na zawadi za ziada ambapo wateja wanne wenye bahati watajishindia magari mapya aina ya SUZUKI SPRESSO na kutakuwa na zawadi nyingine kwa wanaonunua tiketi kwa muda maalum hadi shilingi elfu 15.

 

 

“Kama tulivyosema awali, Tusua Mapene inatoa zawadi mbalimbali kila siku, kila wiki na pale mchezaji atakaponunua tiketi kwa siku na muda maalum.

 

 

“Tangu kuanza kwa shindano, ‘Tusua Mapene’  imekuwa na idadi kubwa sana ya wachezaji na imeshatoa zawadi zenye zawadi zenye thamani ya shilingi bilioni 4.8 kwa washindi wote 421,521 tangu kuanza kwake mwaka 2017,” alisema Kamando.

 

 

Msimu mpya wa Tusuma Mapene unaanza rasmi leo na inategemewa kuwa na zawadi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.4 zitakazogawiwa kwa washindi zaidi ya 300,000 kwa muda wote wa shindano.

 

 

Kushiriki ni rahisi sana, kuna namna mbalimbali ziliandaliwa ili kuwezesha wateja wa kampuni hiyo kushiriki kwa urahisi zaidi, mteja anaweza kutuma ujumbe mfupi wenye herufi  “V” kwenda namba 15544 au kupitia menyu USSD ambapo atabofya *149*01# halafu atachagua vifurushi au kwenye M-Pesa ambapo atabofya *150*00# halafu atachagua namba 6 kisha kifurushi cha chaguo lake.

 

Gharama kwa kila tiketi ni shilingi 300 au mteja anaweza tiketi kupitia M-Pesa ambapo atanunua kwa bei ya punguzo (shilingi 500 kwa tiketi mbili za siku moja, tiketi saba za wiki kwa shilingi 1,800 ama kifurushi cha mwezi chenye tiketi 30 kwa shilingi 6,000) ambapo pia kuna ofa kwa mteja anayenunua tiketi za Tusua Mapene kwa mara ya kwanza ambapo atapata tiketi mbili za bure, anapotuma ujumbe mfupi wenye neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544.

 

Kuhusu Vodacom Tanzania PLC

Vodacom Tanzania PLC ni kampuni inayoongoza ya teknolojia na mawasiliano ikiwa na mtandao wenye kasi kubwa zaidi na data nchini.

 

Tunatoa huduma za mawasiliano kwa wateja zaidi milioni 15. Vodacom Tanzania na kampuni tanzu zake ni sehemu Vodacom Group ya nchini Uingereza. Imesajiliwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ikiwa na namba ya usajili ISIN:TZ1886102715 Jina la Hisa: VODA

Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu : www.vodacom.co.tz     

Leave A Reply