The House of Favourite Newspapers

Vodacom, TECNO Wazindua Simu ya TECNO Camon 11 (Picha + Video)

Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (wa pili kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu mpya ya Tecno Camon 11Pro,  mhamasishaji wa Tecno Abdallah Sultan ‘Dullivan’ wakati wa uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika jana  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Maduka ya rejareja ya Vodacom, Happiness Macha na Meneja Uhusiano wa Tecno Erick Mkomoya (kulia).

 

VODACOM, kampuni nambari moja ya mawasiliano ya simu nchini imeungana na kampuni ya Tecno kuwaletea wateja wao toleo jipya la simu aina ya Tecno Camon 11, jana  jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu ni harakati ya Vodacom kuhakikisha jitihada zake za kuwezesha maisha ya kidijitali kwa wateja wao,  kupitia simu janja zinafanikiwa.

 

Akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa simu hiyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Bw. Eric Mkomoya alisema:

“Tumedhamiria kuhakikisha kila Mtanzania anamiliki simu janja na kwa pamoja tunalifanya taifa la Tanzania kuwa la kidigitali”.

Uzinduzi huu uliohudhuriwa na wateja lukuki utawawezesha watumiaji wa matoleo ya awali wa simu za TECNO Camon kuweza kubadili simu zao ili kujipatia toleo hili jipya kwa kuongeza kiasi kidogo cha pesa.

Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (katikati) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) simu mpya ya Tecno Camon 11pro wakati wa uzinduzi wa simu hiyo akiwa na Happiness Macha na Erick Mkomoya.

Simu hii inapatikana kwa bei ya shilingi laki nne tu (Sh. 400,000) na inakuja na Intaneti ya GB 15 ambapo mteja anapata GB tano kwa miezi mitatu mfululizo. TECNO Camon 11 ina kamera ya mbele yenye uwezo wa mega pixel 16 na kamera mbili za nyuma yenye uwezo wa mega pixel 13 na 2 kwa picha bora zaidi. Simu hii pia ina uwezo wa 4G LTE pamoja na uwezo wa kuhifadhi laini mbili za simu.

 

Pamoja na hayo, simu hii ina flashi iliyotengenezwa kwa rangi maalumu kuweza kusaidia mwanga kutoka vizuri huku ikiwa na kioo chenye ukubwa wa inchi 6.2 chenye uwezo wa FHD. Maduka yote ya TECNO yatatoa si huduma za TECNO tu bali pia kusajili laini za Vodacom.

 

“Tunafurahi kushirikiana na TECNO kuendelea kuimarisha zaidi azimio letu la kuzidi kuwawezesha wateja wetu kuwa katika ulimwengu wa kidijitali. Uzinduzi huu umekuja katika kipindi muafaka, hasa kwa kuwa Watanzania wengi zaidi wanatumia huduma za simu janja,” alisema Jacquiline Materu, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania.

Katika zama hizi za kidigitali, kupata taarifa, kununua na kulipia vitu, na kupata burudani za muziki na sinema, vinawezekana kwa kutumia simu janja, na toleo hili jipya kutoka TECNO litawezesha hayo yote na zaidi.

“Uzinduzi huu umekuja sambamba na msimu wa sikukuu ili kuhakikisha wateja wetu, ambao ndiyo kipaumbele chetu wanasherehekea msimu huu kidigitali zaidi,” aliongeza Materu.

 

Kwa sasa, wateja wote wenye matoleo ya zamani ya TECNO Camon wanaweza kutembelea maduka ya Vodacom na TECNO jijini Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na mikoa mingine saba nchini ili kubadilisha simu hizo na kupata simu mpya ya TECNO Camon 11.

“Nimefurahi sana kupata simu hii, nimebadilisha simu yangu ya TECNO Camon CX na sasa nitasheherekea mwezi wa Desemba na marafiki zangu tukifurahia picha na kumbukumbu bila wasiwasi wa ubora wake. Ninawashukuru sana TECNO na mtandao wangu wa Vodacom,” alisema Hawa

Comments are closed.