The House of Favourite Newspapers

Vodacom Tanzania Foundation Kuwezesha Wanawake 1000 Kutibiwa Saratani

1

????????????????????????????????????Wakina mama wanaotibiwa ugonjwa wa kansa ya kizazi katika hospitali ya Ocean road wakifurahia jambo na Mkuu wa Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kulia) baada ya kutangaza mfumo wa kusaidia matibabu kwa kina mama hao  ulioshirikisha taasisi za T-MARC Tanzania, Pink Ribbon Red Ribbon na Vodacom Foundation ambayo imetoa kiasi cha Dola za Marekani 87,400 kwa ajili ya kuwawezesha akina mama waishio vijijini wanaosumbuliwa na Kansa ya kizazi kuweza kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali pamoja na matibabu ya ugonjwa huo katika hospitali ya Ocean Road (ORCI).

????????????????????????????????????

Baadhi ya akina mama wanaotibiwa ugonjwa wa kansa ya kizazi katika hospitali ya Ocean road, wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliohusu taasisi zisizo za kiserikali za T-MARC Tanzania, Pink Ribbon Red Ribbon na Vodacom Foundation  wakitangaza mfumo wa kusaidia matibabu kwa wakina mama hao  ulioshirikisha taasisi hizo   ambapo  Vodacom Foundation imetoa kiasi cha Dola za Marekani 87,400 kwa ajili ya kuwawezesha wakina mama waishio vijijini wanaosumbuliwa na Kansa ya kizazi kuweza kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali pamoja na matibabu ya ugonjwa huo katika hospitali ya Ocean Road(ORCI).

Saratani ni moja ya ugonjwa ambao umekuwa ukiongezeka kwa kasi nchini katika miaka ya karibuni ambapo umekuwa ukisababisha  watu wengi kupoteza maisha huku wahanga wengi wa ugonjwa huo wakiwa hawajui wafanye nini  zaidi ya kuishi kwa hofu , wengi wakiwa hawajui dalili zake na wanaozijua wakiwa wanaamini kuwa hauna tiba .

Ugonjwa wa Saratani umekuwa ukiwashambulia binadamu kupitia aina mbalimbali za viungo vyao na matibabu yake yamekuwa yakitofautiana kadri ya ugonjwa unavyokuja .

Kwa hapa nchini Saratani ya Shingo ya kizazi ambayo imekuwa ikiwashambulia wanawake ni tishio kubwa na  imekuwa ikisababisha vifo vingi.Tafiti za karibuni zinabainisha kuwa kati ya wanawake wahanga wa ugonjwa wa Saratani nchini,asilimia 55 hadi 65 wanasumbuliwa na saratani ya shingo ya kizazi na inakadiriwa kuwa kati ya wanawake 7,515 wanaobainika kuwa na  ugonjwa huu kwa mwaka   idadi yao kubwa yaani 6,009 hupoteza maisha.

Changamoto  nyingine kwa wanawake wahanga wa ugonjwa huu inayopelekea wachelewe kupata matibabu imebainishwa kuwa ni kuwa na maisha duni ambapo wengi wao wanakuwa hawana uwezo wa kusafiri hadi kwenye hospitali kubwa  zinazofanya uchunguzi na matibabu , matokeo yake wengi  huishia kubaki majumbani kwao hususani maeneo ya vijijini hadi wanapofikwa na mauti ya kifo.Zaidi ya asilimia 95 ya wanawake wahanga wa Saratani ya Shingo ya kizazi nchini wanakabiliwa na tatizo hili.

Katika kupunguza vifo vya akina mama kutokana na Saratani ya Shingo ya kizazi, taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ya T-Mark na Pink Ribbon Red Ribbon yameamua kulivalia njuga tatizo hili kwa kuanzisha mradi unaotoa elimu kwa akina mama kujua dalili za ugonjwa huo na kuwawezesha kusafiri bure kutoka makwao hadi jijini Dar es Salaam ilipo hospitali inayotoa matibabu ya Saratani ya Ocean Road  na Bugando ili wakatibiwe.

Kupitia huduma ya  M-Pesa wanawake waliofanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa na dalili ya Saratani ya shingo ya kizazi huweza kupata fedha za nauli kutoka kwa washirika wa Vodacom Foundation katika utekelezaji wa mradi huu ambapo  huweza kufika kwenye hospitali kwa ajili ya matibabu.Katika kipindi cha miaka 5 mradi huu umelenga kuwafikia wanawake  zaidi ya 1,000 ambao watapatiwa nauli kutibiwa katika hospitali 2 za Bugando na Ocean Road.

1 Comment
  1. Deborah says

    Hadithi.. . . . …!?

Leave A Reply