The House of Favourite Newspapers

Vodacom Watoa Bima za Afya 200 Kwa Wanawake, Watoto na Zawadi Kibao

0

Vodacom yakabidhi bima kubwa ya bure kwa akina mama na watoto wachanga 200 kupitia VodaBima pamoja na zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu ya shilingi milioni 10 visiwani Zanzibar.

Mshindi wa pesa taslimu shilingi milioni 10 kupitia kampeni ya Vodacom Tanzania PLC inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, Bi. Lulu Kadege (kulia) akiwa ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa na Masta Shangwe katika viwanja vya Kisonge visiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii wateja wanayo fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
Masta Shangwe akikabidhi simujanja kwa mshindi aliyepatikana kupitia kampeni ya Vodacom Tanzania PLC inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, aliyokabidhiwa katika viwanja vya Kisonge visiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii wateja wanayo fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
Masta Shangwe (aliyevaa kofia ngumu katikati) akiwa na Meneja Mauzo visiwani humo, Fadhili Linga (kulia) akikabidhi kiashiria cha bima ya afya kwa mmoja wa akina mama katika hospitali ya Mnazi Mmoja mwishoni mwa wiki Zanzibar kupitia kampeni inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’. Kupitia kampeni hii jumla ya akina mama na watoto wachanga 2,000 watakabidhiwa bima kubwa ya afya kupitia VodaBima kutoka Vodacom itakayotumika kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kampuni hiyo kwenda kwa watanzania katika msimu huu wa sikukuu.

 

Leave A Reply