The House of Favourite Newspapers

Vodacom, WCB waja na Tamasha la ‘Nogesha Upendo’

003-nogesha-upendo

Baadhi ya wasanii wa nembo ya WCB wakiongozwa na Diamond Platinumz wakiwasili katika makao makuu ya Vodacom Tanzania, yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la “Nogesha Upendo” litakalofanyika Desemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Desemba 25 Iringa katika Uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.

001-nogesha-upendo

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyomella (kushoto) akimsikiliza Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kutanga tamasha la “Nogesha Upendo” yatakayofanyika Desemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Desemba 25 Iringa katika uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.

002-nogesha-upendo

Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz (katikati) akipiga selfie na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania mara baada ya mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tamasha la “Nogesha Upendo” litakalofanyika Desemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Desemba 25 Iringa katika Uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.

DAR ES SALAAM: Katika mwendelezo wake wa kuwapatia wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla burudani za sikukuu, Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wasanii wa WCB imeandaa matamasha mawili ya kukata na shoka ambayo yatafanyika katika msimu huu wa sikukuu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyomella, alisema matamasha hayo makubwa ya muziki wa kizazi kipya yatafanyika katika mikoa ya Dar e salaam na Iringa chini ya wasanii Diamond Platinumz, Rayvanny , Rich Mavoko, Harmonize na Queen Darleen.

“Kama mnavyoelewa msimu huu huwa umeambatana na shamrashamra mbalimbali za sikukuu na mitoko ukiwa na familia yako, Desemba 24 kutashushwa shoo ya Nguvu katika fukwe za Jangwani Sea Breeze Hotel ambapo kutakuwa na tamasha la kihistoria la “Vodacom Wasafi Beach Party” na Iringa tamasha litafanyika siku ya Krismasi katika uwanja wa Samora na Matamasha yote yataanza saa nane mchana”.Alisema.

Mwiyombella alisema burudani hii ya muziki inakwenda sambamba na promosheni ya Nogesha Upendo ya http://vda.cm/nogeshaupendo Vodacom inayolenga kuwapatia wateja wote wa mtandao wa Vodacom zawadi za sikukuu ikiwa ni shukrani kwa wateja ambapo pia wateja wanayo fursa ya kujishindia tiketi za bure za kushiriki katika matamasha haya makubwa katika msimu huu wa sikukuu.

“Ili kujishindia tiketi ya bure anachotakiwa kufanya mteja wa Vodacom ni kupiga *149*01# kisha nunua kifurushi chochote cha Vodacom na moja kwa moja utakua umeingia katika droo ya kuweza kujishindia tiketi yako. Zawadi nyingine kemkem kupitia promosheni ya Nogesha Upendo ni fedha taslimu, muda wa maongezi, Vifurushi vya intaneti (Mb).” Alisema.

Naye Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetamba katika anga za kimataifa, Diamond Platinumz akiongea kwa niaba ya wasanii wa WCB alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Iringa kujitokeza kwa wingi siku ya shoo hizo kwani zitakuwa ni shoo za kihistoria katika mikoa hii miwili kufanywa na Vodacom kwa kushirikiana na WCB, Napenda kuwahakikishia mashabiki wetu kwamba tutakamua vilivyo tukiwa na wasanii wenzangu wote wa WBC kwa “Kunogesha Upendo” Alisisitiza Diamond.

Comments are closed.