The House of Favourite Newspapers

Vodacom yaja na simu mpya ya bei nafuu

0

voda 2Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa  uzinduzi wa simu mpya aina ya Alcatel mwishoni mwa wiki yenye vioo 2, kamera, radio, MP 1.3, kadi yenye GB 16 na betri  yake inayotunza chaji  kwa muda mrefu. Simu hiyo inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa Tsh.20,000 tu, Kulia ni Meneja wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo, Edwin Byampanju.
vodaMeneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) na Meneja wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo, Edwin Byampanju wakionesha simu mpya aina ya Alcatel kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu hiyo mwishoni mwa wiki. Simu hiyo ina vioo 2,kamera,radio,MP 1.3, na kadi yenye GB 16 na betri inayotunza chaji  kwa muda mrefu zaidi.

Katika mwendelezo wake wa kufanya maisha ya watanzania kuwa murua na kuwapeleka katika karne ya sayansi na teknolojia, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imezindua simu ya mkononi ya gharama nafuu kabisa ambayo haijawahi kutokea nchini.

Simu hiyo  aina ya Alcatel ambayo bei yake ni nafuu ya shilingi 20,000/- imeanza kusambazwa sehemu mbalimbali nchini na itapatikana katika maduka ya Vodacom na mawakala wake wote nchini kote hususani maeneo ya vijijini.

Akiongea kuhusu uzinduzi wa simu hii mpya,Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema “Vodacom imeingiza simu hii ya gharama nafuu ambayo imetengenezwa kumuwezesha mtumiaji kupata huduma mbalimbali na dhamira yetu kubwa ni kuendelea kufanya ubunifu wa kiteknolojia wa kurahisisha maisha ya watumiaji wa simu pia kuwapeleka katika ulimwengu wa teknolojia”.Alisema.

Alisema kwa mwaka huu kampuni itaendelea kubuni huduma mbalimbali  za kurahisisha mawasiliano dhamira yake kubwa ikiwa ni kuhakikisha kila mtanzania ameunganishwa kwenye mtandao na anafurahia maisha kupitia teknolojia ya simu.

Nae Meneja wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Edwin Byampanju aliielezea simu hiyo kuwa ina uimara mkubwa, ina kioo chenye ukubwa wa inchi 2 na mwonekano wa mbele wenye rangi maridhawa,ina kamera yenye ukubwa wa MP 1.3, betri inayotunza chaji  kwa muda mrefu zaidi ya siku tano,ina redio pia inao uwezo wa kutumia kadi ya kumbukumbu hadi GB 16”.

Aliwataka wateja wote wanaotumia mtandao wa Vodacom kuchangamkia fursa ya kumiliki simu imara na yenye ubora wa kisasa kwa gharama nafuu na kuendelea kupata huduma bora zinazorahisisha maisha.

Leave A Reply