The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yawapongeza Wateja Wake

Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania, Linda Riwa (kulia) akinyanyua juu Champagne kuzinduzi rasmi wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika kwenye duka la Voda makao makuu jijini Dar Es Salaam leo. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom, Harriet Lwakatare.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare akizungumza na waandishi na wateja waliohudhuria siku ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania, Pia alitoa shukurani kwa wateja na wafanyakazi wa Vodacom kwenye wiki hii na alitoa wito kwa wateja wasajili laini zao kwa alama ya vidole kote nchini. Kulia ni George Lugata, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare akimlisha keki mmoja kati ya wateja waliokuwepo dukani siku ya leo.

Comments are closed.