The House of Favourite Newspapers

Volkano yaibuka Indonesia siku chache baada ya tetemeko la ardhi, tsunami

KUIBUKA kwa volkano katika Mlima Soputan, katika kisiwa cha Sulawesi nchini Indonesia, kunafuatia siku chache baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa ‘magnitude’ 7.5 na tsunami kukikumba kisiwa na jiji la  Palu na kuua watu zaidi ya 1,300.

Volkano hiyo iliibuka jana katika kisiwa hichohicho na kuua watu zaidi ya 1,4000.

Mlipuko huo uliifanya serikali  kutoa onyo kwamba uwezekano wa kurushwa kwa matope ya moto (lava) na moshi wa majivu vinaweza kuhatarisha usafiri wa anga.

Pia imetolewa amri ya kuwahamisha watu waliomo katika eneo linaloweza kufikiwa na athari ya volkano hiyo.  Mlipuko huo ulirusha majivu angani hadi kufikia urefu wa mita 6,000.

Wanasayansi bado hawajapata uhakika iwapo kuibuka huko kwa volkano kunahusiana moja kwa moja na  tetemeko lililokuwa limetokea siku kadhaa nyuma.

Indonesia ina maeneo mengi yaliyo na volkano ‘inayochemka’ ardhini.  Pia ipo katika ukanda uitwao “Ring of Fire” (Duara la Moto), ambalo ni moja ya maeneo yanayokumbwa zaidi na matetemeko ya ardhi.

Rais wa Marekani, Donald Trump, alimpigia simu Rais wa Indonesia,l  Joko “Jokowi” Widodo, jana akimwahidi kuipatia misaada ya dharura nchi yake na kusaidia katika kuijenga upya baada ya kukumbwa na tetemeko na tsunami eneo la  Sulawesi.

                                

Pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vifo katika tukio la wiki iliyopita, mamia ya watu walijeruhiwa vibaya, ambapo mabarabara na njia za mawasiliano ziliharibiwa vibaya, ikiwa ni pamoja na kusababisha uhaba na uharibifu wa chakula, maji, mafuta na ukosefu wa dawa.

Kwa mujibu wa Shirika la Taifala  Kushughulikia Majanga nchini Indonesia, mji wa Palu umeharibiwa vibaya ambapo watu zaidi ya 60,000 hawana mahali pa kuishi kufuatia makazi yao kuharibiwa.

Comments are closed.