The House of Favourite Newspapers

Waajiri Wanaodaiwa NSSF, PSSF Kimeumana

0

 

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, amewaagiza Mameneja wa Mikoa NSSF, PSSF na Compliance Officers kuhakikisha kuwa hakuna madeni kwa waajiri na waajiri wenye madeni wachukuliwe hatua.

 

Katambi amesema hatua hii ni kutokana na kuwepo kwa waajiri ambao wamekuwa wakileta ujanjaujanja na unapofika muda wa kustaafu mfanyakazi anasumbuliwa pesa zake za mafao.

 

“Hili la wadaiwa sugu au waajiri sugu wasiolipa mishahara, kodi (P.A.Y.E) na michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii tutawatangaza kumi bora hadharani na kuwapa tuzo ya hati chafu ya Kutotii Sheria za Kazi…”

 

“Natoka shukrani za dhati kwa niaba ya Waziri Mkuu wetu Kasimu Majaliwa na Waziri wa Nchi Jenista Mhagama kwa TUCTA na ATE kwa ushirikiano wao mkubwa na kusimamia haki za Wafanyakazi wa Tanzania,” amesema Katambi.

 

Leave A Reply