Waandishi wa Habari Wapigwa Msasa Ishu ya Nishati Jadidifu

Waandishi wa habari wakinolewa kwenye semina kuhusu nishati jadidifu (renewable energy)

Semina ikiendelea

Wadau wakifuatilia semina hiyo. Kulia ni mwandishi wa mtandao huu, Hashim Aziz na Injinia wa Nishati Viwandani, Winniefrida

Mjumbe akichangia hoja.

Wawakilishi wa shirika la Hivos kutoka Kenya wakifuatilia semina hiyo. Kushoto ni Maimuna Kabatesi, Advocacy Officer wa Hivos.

Wajumbe wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.

 

Tanzania Media Foundation (TMF) kwa kushirikiana na shirika la mazingira kutoka Kenya, Hivos wameandaa semina maalum ya kuwaelimisha waandishi wa habari juu ya namna ya kufuatilia na kuripoti habari zihusuzo nishati jadidifu (renewable energy) hususan katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Semina hiyo ya siku mbili, imeanza leo, Agosti 3, 2017 katika Hoteli ya Protea Courtyard, Upanga jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, wadau wa sekta ya nishati na mazingira kutoka Tanzania na wengine kutoka nchini Kenya.

Semina hiyo ya siku mbili, ina lengo la kuangazia matatizo yanayoikumba sekta ya nishati ukilinganisha na mabadiliko ya hali ya hewa, ikiwemo mbinu za kuhakikisha nishati inawafikia kwa urahisi hata watu walioko vijijini ambao wana uhitaji mkubwa.

Na Hashim Aziz/ GPL

Toa comment