The House of Favourite Newspapers

Waangola Kuihukumu Yanga

KUELEKEA mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, Waamuzi kutoka nchini Angola wanatarajiwa kuchezesha mchezo wa Yanga dhidi ya Rayon Sports utakaopigwa Mei 16, mwaka huu.

 

Yanga inatarajiwa kuvaana na Rayon mnamo Mei 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, saa moja usiku katika mwendelezo wa mechi za makundi baada ya ule wa awali dhidi ya U.S.M Alger ya Algeria.

 

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema waamuzi hao kutoka Angola ndiyo watasimamia mchezo wa Yanga wa Mei 16.

 

“Waamuzi hawa kutoka Angola ni Helder Martins Rodrigues De Carvalho akisaidia na Ivanildo Meirellers De O Sanche Lopes, Wilson Valdmiro Ntyamba, Joao Amado Muanda Goma huku mechi kamishina Abebe Solomon Gibresilassie akitokea Ethiopia.

 

“Pia msimamizi wa jumla wa mchezo huo atakuwa ni Yoland Mavouroulou wa Gabon, upande wa vyombo vya habari atasimamia Clifford Ndimbo kutoka Tanzania,” alisema Ndimbo.

 

Wakati huohuo, Kikosi cha Ngorongoro Heroes ambacho kinatarajiwa kucheza Mei 13, mwaka huu kimeongeza wachezaji wawili katika kikosi chake.

 

Wachezaji hao ni Peter Dotto Mashauri wa Black Sailor aliyechukua nafasi ya Ramadhani Kabwili wa Yanga na Nasri Daud kutoka kituo cha Bitebo Aspire (Senegal).

Comments are closed.