The House of Favourite Newspapers

Waarabu Wa Qatar Wataka Kuinunua Manchester United Watoa Ofa

0

THE Group of Qatari ni wawekezaji ambao wapo tayari kwa ajili ya kuinunua Manchester United huku wakiamini hakuna ambaye atatoa ofa kubwa kwa klabu hiyo kongwe ya Premier League.
Familia ya Glazer ambao kwa sasa ndiyo wamiliki wa Manchester United wapo bize kusaka mteja mpya kwa ajili ya klabu hiyo na walitoa muda wa mwisho ambao katikati ya Februari hii kwa ajili ya kuiuza klabu.

Ripoti zinaeleza kuwa kundi la matajiri binafsi kutoka Qatar wanajiandaa kutoa ofa kubwa katika siku zijazo na wapo tayari kutoa fedha za bajeti ya usajili kwa kocha Erik ten Hag kama dili lao litafanikiwa la kuichukua United.The Qatari group sio kundi pekee wapo tayari kuinunua Manchester United lakini kun Jim Ratcliffe naye aliweka wazi malengo ya kutaka kuinunua timu hiyo.

Huyu ni bilione na tajira ambaye amekuwa shabiki wa United na huenda akawa hata chaguo la mashabiki, ingawa ofa ya Qatar inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko yake.

Atakayefanikiwa kuinunua Manchester United anatakiwa kujipanga kwani familia ya Glazer inahitaji kiasi cha pauni 6 bilioni.

Hata hivyo kutakuwa na kazi kubwa kwa mmiliki ajaye katika kuifanya marekebisho Old Trafford au kujenga uwanja mpya.

TUNDU LISSU ATINGA KITUO CHA POLISI DODOMA KUFUATILIA GARI LAKE – “NATAKA KULIPELEKA MAKUMBUSHO”

Leave A Reply