The House of Favourite Newspapers

Wabunge CUF Wadai Viti Vyao Bungeni

0

WABUNGE wanane wa viti maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF), walioshinda kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Novemba 10 mwaka huu wamemwandikia barua Spika wa Bunge John Ndugai ya kutaka warejeshwe kazini.

Wabunge hao wanaomuunga mkono katibu mkuu Maalim Self Sharif Hammad katika chama hicho chenye mgogoro, walidaiwa kufukuzwa uanachama na CUF na upande wa mwenyekiti Profesa Ibrahimu Lipumba katikati ya mwaka huu.

Prof. Lipumba anatambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kama mwenyekiti halali wa chama hicho, na kwa msingi huo barua kutoka upande wake kwenda kwa Spika ilikubaliwa na Ndugai Julai 26.

Lakini wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wabunge hao walisema baada ya kutoka kwa hukumu ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Lugano Mwandambo, ambayo iliwarudishia uanachama wao waliandika barua kwa Spika wa Bunge kuomba kurudishiwa ubunge wao kwa sababu ni wanachama halali wa CUF.

 

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, aliyekuwa Mwenyekiti wa Wabunge wa chama hicho, Riziki Shahari Mngwai, alisema waliandika barua hiyo Novemba 20 kupitia kwa Katibu wa Bunge.

Baada ya Ndugai kukubaliana na maamuzi hayo ya CUF Lipumba, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Septemba 5 ilitangaza wabunge wapya wa viti maalum kutoka upande wa Prof. Lipumba.

Mahakama Kuu iliona upande wa CUF Lipumba ulikosea kuwavua uanachama walalamikaji wanane hao.
“Tunaamini kwamba baada ya mahakama kuu kutenda haki, uamuzi huo utaheshimiwa,” alisema Riziki.
Nipashe jana ilimtafuta Spika Ndugai kupitia simu yake ya mkononi kwa ajili ya kufahamu kama imefika mezani kwake lakini haikupokelewa.

Baadaye Ndugai alituma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) akiomba ajulishwe lolote kwa njia hiyo. Hata hivyo, hakujibu ujumbe alioandikiwa kupitia simu yake ya mkononi.

CHANZO: IPP MEDIA

FULL Stori ipo hapa

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply