The House of Favourite Newspapers

Wabunge DRC Kupiga Kura Kumwondoa Spika

0
                Spika, Jeanine Mabunda, ambaye anatoka chama cha rais wa zamani wa DRC. Joseph Kabila.

ZAIDI ya wabunge mia mbili kati ya wabunge mia tano wameanza kikao cha kupiga kura ya  kumwondoa madarakani Spika wa bunge, Jeanine Mabunda, kutoka chama cha Joseph kabila.

 

Wabunge wa upande wa rais aliye madarakani, Felix Tschisekedi, wanamtuhumu Mabunda  kwa uongozi mbaya.

 

Kwa mujibu wa mbunge Moindo Nzangu, ambaye aliwasilisha mapendekezo ya kura hiyo  Mabunda atatakiwa kujitetea mbele ya wabunge kabla ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

 

Kikao hicho ambacho kilipangwa kuanza saa nne asubuhi leo Desemba 10, kimechelewa kutokana na msako na ulinzi mkali uliofanywa na vikosi vya usalama ndani ya bunge.

 

Vurugu na ghasia zilitokea ndani ya bunge hilo wiki hii, wakati ulipowasilishwa muswada wa kura ya maoni na watu kadhaa walijeruhiwa wakati wanaharakati na wabunge walipoanza kurushiana viti, na kuharibu samani ndani ya bunge.

 

Mzozo wa hivi karibuni wa kisisiasa nchini Congo, umeibuka tena baada ya Rais Félix Tshisekedi kutangaza nia yake ya kuvunja bunge ili apate wingi wa wabunge ambalo kwa sasa lina idadi kubwa zaidi ya wabunge kutoka chama cha mtangulizi wake rais mstaafu, Joseph Kabila.

 

Leave A Reply