The House of Favourite Newspapers

Haji Manara Kuchukua Jiko Leo

0

MSEMAJI wa Klabu ya Simba, Haji Manara, mapema jana amethibitisha kuwa ifikapo siku ya leo Alhamisi, Desemba 10, 2020,  anatarajia kufunga ndoa na mchumba wake aliyemtambulisha kwa jina Naheeda.

 

Amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba ndoa hiyo itafungwa katika msikiti wa Maamur na sherehe zitaendelea  jijini Dar es Salaam hadi siku ya Jumamosi.

 

“Watu wangu wa nguvu karibuni katika harusi yangu itakayofungwa kesho Masjid Maamur na katika sherehe mbalimbali zitakazofanyika hapa Dar Inshaallah!!

 

“Lakini kubwa kwa wale wasiokuwa-invited kuangalia tafrija kubwa itayorushwa live na Channel ya Sinemazetu ya Azamtv, tokea katika hoteli ya Serena siku ya Jumamosi!!

 

“Naomba dua zenu ndoa yetu iwe ya kheri na tuishi kwa amani na furaha mm na Laaziiz wangu kipenzi Naheeda.” ameandika mtandaoniManara.

Leave A Reply