The House of Favourite Newspapers

Wabunge Walalamikia Kondom Feki

0

WABUNGE nchini Zambia wamelalamikia kondom na glovu zisizo na viwango zinazosambazwa na Kampuni ya Honey Bee, ikidaiwa zinaweza kuvuja zikijazwa maji, hali ambayo imeleta hofu kwa wananchi kwa kuwa zilianza kutumika Septemba, 2020 huku akifananisha kitendo hicho sawa na ‘mauaji ya Kimbari‘.

 

Glovu kutoka kampuni hiyo ya nchini Zambia zilipangwa kutumika na watumishi wa afya kuwahudumia wagonjwa wa COVID-19. Uchunguzi ulibaini zabuni ya kandarasi hiyo haikutolewa kwa utaratibu mzuri, kwani ilitolewa Jumapili ambayo siyo siku ya kazi 

 

‘’Kile ambacho wizara ya afya inakifanya ni mauaji ya kimbari. Unapoweka maji katika glovu hizo na mipira ya kondom zinavuja. Ni watu wangapi wamefariki kuanzia mwezi Septemba kutokana na uzembe huu,’’ alisema mbunge Mwansa Mbulakulima.

 

Mbunge huyo alisema kwamba ana wasiwasi kuhusu usambazaji wa magonjwa ya zinaa na virusi vya corona.

 

‘’Glovu hizo zinapaswa kutumika na wafanyakazi wa afya wanaokabiliana dhidi ya virusi vya corona na zimesambazwa kote nchini licha ya kuwa na hitilafu,’’ alisema Mbulakulima.

 

Mkurugenzi wa Imran Lunat aliishutumu ofisi ya mkaguzi mkuu kwa kuwa na upendeleo katika ripoti yake ilipobaini kwamba kampuni hiyo haina ofisi ya moja kwa moja kulingana na ripoti ya gazeti la serikali Daily Mail. Ukaguzi huo pia ulibaini kwamba kandarasi hiyo ilitolewa siku ya Jumapili ambayo siyo siku rasmi ya kazi.

 

Kakulubelwa Mulalelo, katibu wa kudumu katika wizara hiyo aliiambia kamati kwamba hana ufahamu ni nani aliruhusu kutolewa kwa kandarasi hiyo, na kwamba yeye alihudhuria uzinduzi na usambazaji wa bidhaa hizo pekee.

 

Raia wa Zambia kwenye mtandao wa Twitter wametoa maoni yao kutokana na tatizo hilo.


Leave A Reply