The House of Favourite Newspapers

Wabunge Wavurugana Tena bungeni Nchini Kenya

wabunge-kenyaNAIROBI, KENYA: Wabunge wa upinzani nchini Kenya wametoka bungeni kwa hasira mapema leo asubuhi desemba 22, 2016 katika Mji Mkuu wa Nairobi nchini humo kwa madai kuwa baadhi yao wamekuwa wakinyanyaswa

Kikao hicho maalum ambacho vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia kilitarajiwa kupigia kura marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambayo inaruhusu kuhesabiwa kwa kura moja baada ya nyingine katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwakani.

Serikali inataka mfumo ambao utasaidia shughuli ya kuhesabu kura iwapo mfumo wa kielektroniki utafeli lakini upinzani unasema kuwa ni njia moja wapo ya kuiba kura.

Awali hatua ya kuupigia kura mswada huo ili ufanyiwe marekebisho ilisababisha kuzuka kwa ghasia juzi, Jumanne.

Upinzani wa CORD umesema kuwa mmoja ya wabunge wake aliumizwa hadi kuvuja damu usoni kufuatia vurugu na wabunge wa chama tawala mapema siku ya Jumatano.

Cord imeenda mahakamani ikitaka marekabisho hayo kutopitishwa bungeni lakini chama tawala kimepitisha marekebisho hayo.

Serikali Yaingilia Kati Suala la Parking

 

Comments are closed.