The House of Favourite Newspapers

Wachezaji 29 Zanzibar Waingia Kambini Kuiwinda Stars

0

JUMLA ya wachezaji 29 wa kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes jana Jumapili waliingia kambini kwa ajili ya kuanza kujiwinda na mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kikosi hicho kimeingia kambini kwa ajili ya mchezo huo ambao ni maalum kwa ajili ya uzinduzi wa Uwanja wa Amaan, visiwani hapa ambao utapigwa keshokutwa Jumatano.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) Kibabu Haji amesema kuwa kikosi hicho kitanolewa na kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ akisaiwa na Ali Suleiman Mtuli na Saleh Ahmed Machupa akiwa kocha wa makipa.

Baadhi ya nyota ambao walitarajiwa kuingia kambini ni pamoja na makipa; Ahmed Ali Suleiman (Uhamiaji), Ibrahim Abdallah Rashid (Singida Fountain Gate), Yakoub Suleiman Ali (JKU)

Kwa upande wa mabeki wapo Adeyum Saleh Ahmed (Dodoma Jiji), Abdallah Said (Mlandege), Abdul-Malik Adam Zakaria (Namungo), Mukrim Issa Abdallah (Singida Fountain Gate), Ibrahim Hamad ‘Bacca’ (Yanga SC), Baraka Mtuli (Mashujaa FC) na Suwed Juma (JKU SC).

Viungo wapo Suleiman Ame Awesu (Zimamoto), Is-haka Said Mwinyi (KMKM), Hassan Nasoor (JKT Tanzania), Shekhan Ibrahim (Yanga), Feisal Salum (Azam), Nasir Sheha Abdallah (KMKM) huku washambuliaji wakiwa Matheo Antony (Mtibwa), Maabad Maulidi Maabad (Coastal union) na Abdul Nasir Assa (Mashujaa).

Kazija Thabit, Zanzibar

Leave A Reply