Wachezaji wa Simba walivyokutana na bil 11.5

VITA Club ambayo inacheza na Simba Jumamosi usiku jijini Kinshasa, imetenga bajeti ya Sh11.5 bilioni kwa msimu mzima wa 2018/19. Klabu hiyo ni miongoni mwa timu tajiri nchini humo kutokana na kuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato huku ikiwa imefanya vizuri mara kadhaa kwenye mashindano makubwa na kupata mamilioni.

 

Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania, wao wamepanga kutumia bajeti ya Sh6 bilioni kwa msimu wa 2018/19 katika mashindano yote chini ya muwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo’.

 

Kwa mujibu wa Katibu wa Vita, Raphael Esabe bajeti hiyo itahusisha michuano ya ndani na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Anasema kwamba fedha hizo ni makadirio kwani wana uhakika wa kupata fedha nyingi zaidi kutokana na ufanisi wao kwenye mashindano mbalimbali wanayoshiriki haswa Ligi ya Mabingwa Afrika. Anasema kikosi cha wachezaji 27 walichonacho ni imara na ana uhakika kwamba kitawatimizia malengo yao ya msimu huu.

Loading...

Toa comment