The House of Favourite Newspapers

Wachina Waishio Tanzania Washerehekea Siku Yao ya Mwaka Mpya

1

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo katika sherehe hizo.

2

Balozi wa China hapa nchini, LU Youging akizungumza jambo kwenye sherehe hizo.

 

3

Baadhi ya sehemu za migahawa za Kichina iliyokuwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

4

5

7

Vikundi mbalimbali vikionesha ujuzi wao kwenye sherehe hizo.

8

Baadhi ya raia wa China waliohudhuria hafla hiyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

9

Vijana raia wa China wakitoa burudani katika hafla hiyo.

 

10

Balozi wa china hapa nchini, LU Youging (kushoto), akimkabidhi hundi ya zaidi shilingi milioni sabini Makamu wa Rais, Samia Suluhu.

11

…burudani zikiendelea katika hafla hiyo.

Raia wa China waishio Tanzania, leo wameadhimisha sherehe ya Mwaka Mpya wa Kichina katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.

Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youging ndiye aliyewaongoza Wachina waishio nchini katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, akiwemo Nape Nnauye, Balozi Augustine Mahiga na wengineo.

Michezo mbalimbali ya Kichina ilikuwa kivutio kikubwa kwenye viwanja hivyo ambapo pia, Balozi wa China alikabidhi hundi ya zaidi ya shilingi milioni sabini ikiwa ni hatua ya kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika ujenzi wa Shule ya Msingi Chato aliyosoma.

Na Denis Mtima/GPL

 

Comments are closed.