The House of Favourite Newspapers

Wachina Waomba Kujenga Uwanja Yanga

0

MEELEZWA kuwa kuna kampuni tisa hadi sasa zimetuma maombi ya kutaka kutengeneza Uwanja wa Yanga uliopo Kigamboni jijini Dar huku moja kati ya kampuni hizo ni kutoka China.

 

Yanga ipo katika mchakato wa kukamilisha ujenzi wa uwanja wake uliopo Kigamboni waliokabidhiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo wanatarajia kujenga uwanja wa nyasi bandia na kawaida.

 

Aidha, klabu hiyo ilitangaza tenda mwishoni mwa mwaka jana ili kupata wazabuni watakaojitokeza kutengeneza uwanja huo.

Taarifa ambayo Championi Ijumaa imeipata kutoka Yanga inasema kuwa tayari wameshapokea maombi kutoka makampuni tisa ambayo yote yanahitaji kujenga uwanja wa Kigamboni ikiwemo kampuni moja kutoka nje ambayo ni ya Wachina.

 

“Awali tulitangaza tenda ambayo mwisho wake ilikuwa mwishoni mwa mwaka jana Desemba lakini tulisogeza mbele kutokana na kuwepo kwa Sikukuu za Krismasi na mwaka mpya ambapo makampuni mengi yalikuwa yamefungwa, hivyo kwa sasa tayari kila kitu kipo wazi hivyo mchakato unaendelea vizuri.

 

“Ushindani umekuwa mkubwa sana kwani kuna makampuni tisa hadi sasa tayari yameshaleta barua kuomba kutengeneza uwanja ambapo kati ya hayo, manane ni ya ndani na moja ya kutoka nje ya nchi ambao ni Wachina.“

 

Uongozi upo katika mchakato wa kuchuja makampuni hayo na kuangalia kampuni ipi itafaa na kukidhi vigezo kuweza kutengeneza uwanja,” alisema mtoa taarifa huyo.

Stori: Khadija Mngwai, Dar es salaam

Leave A Reply