The House of Favourite Newspapers

Waethiopia Wakusanyika Katika Ubalozi wa Urusi Kujiandikisha kwa Vita Nchini Ukraine

0

VIJANA  wa Ethiopia wanaendelea kukusanyika katika ubalozi wa Urusi mji mkuu Addis Ababa, leo Jumanne Aprili 19, 2022 kufuatia uvumi wa kuajiriwa kwa wanajeshi kupigana nchini Ukraine.

Lakini msemaji wa ubalozi huo, Maria Chernukhina, alisema hakuna uajiri unaofanywa nchini Ethiopia.

Alisema watu hao walikuwa wanaonyesha mshikamano na Urusi.

 

“Tuna wageni wengi katika ubalozi huu wanaokuja kuunga mkono Urusi,” alisema  msemaji wa ubalozi huyo

“Baadhi yao wanatuambia wako tayari kusaidia kwa njia yoyote wanayoweza. Lakini sisi sio wakala wa kuajiri,” Bi Chernukhina aliongeza.

Baadhi ya vijana hao wa Ethiopia katika ubalozi huo walionekana wakiwa na hati zao za kibinafsi.

Ethiopia ilikuwa miongoni mwa nchi zilizokosa kikao cha Umoja wa Mataifa cha kupigia kura azimio kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Leave A Reply