The House of Favourite Newspapers

Wafahamu Dada Mapacha Wakongwe Zaidi Duniani

0

 

Dada wawili raia wa Japani wamethibitishwa na kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness World Record kama mapacha wazee zaidi wanaofanana duniani kwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 107 na siku 300 (takribani miaka 108).

Umeno Sumiyama na Koume Kodama wamevunja rekodi iliyowekwa na dada mapacha wa Japani, Kin Narita na Gin Kanie.

Umeno na Koume, wote wanatajwa kama watu wenye kupenda kutengamana na wengine, walizaliwa mnamo Novemba 5, 1913 katika kisiwa cha Shodoshima.

Tangazo la Guinness World Record Book lilitolewa Jumatatu ikiwa ni maadhimisho ya ‘Siku ya Wazee’ ambayo hufanywa kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa nchini Japani.

Kwa sababu ya hali ya sasa na Covid-19, na kama tahadhari, akina dada hao ambao wanaishi katika sehemu tofauti za Japani walitumiwa vyeti vyao rasmi huko huko katika nyumba zao tofauti ambazo wanatunzwa.

Waliokuwa wakishikilia rekodi za awali za mapacha wazee zaidi duniani wanaofanana ni Kin na Gincha waliokuwa na umri wa miaka 107 na siku 175 kabla ya kifo cha Kin mnamo Januari 2000. Gin naye alifariki dunia mwaka uliofuata, akiwa na miaka 108.

Mapacha hao marehemu, ambao majina yao yanamaanisha dhahabu na fedha kwa Kijapani, walikuwa wamezaliwa Agosti mosi, 1892 huko Nagoya, na walikuwa watu mashuhuri kwa vyombo vya habari hasa katika kipindi cha muongo wao wa mwisho wa Maisha yao hapa duniani.

Familia ya Umeno na Koume walisema kwamba dada wote wawili walikuwa walikuwa wakitaniana juu ya kufikia umri wao.

Japani, matarajio ya maisha ni ya juu zaidi ulimwenguni, na watu wazee wanapewa heshima kubwa. Mtu mzima mkongwe zaidi duniani kulingana na kitabu cha Guinness, kwa sasa ni mwanamke wa Japani mwenye umri wa miaka 118, Kane Tanaka (alizaliwa January 2, 1903) mpaka sasa yu hai.

Leave A Reply