The House of Favourite Newspapers

Wafanyabiashara Kariakoo Waendelea Kunufaika na ‘Betika’

0

 

IKIWA ni Jumatano ya kwanza ya Januari 8, 2020, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers Ltd  imeendelea na kulisambaza gazeti la maarufu la Betika ambalo ni mahsusi kwa masuala ya kubeti likiwa pia ni mkombozi wa wafanyabiashara na watu wengine mbalimbali wanaohitaji kutangaza biashara zao ndani yake.

 

Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd na huingia mtaani kila Jumatano.

 

 

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linajihusisha na masuala ya ‘betting’ na ‘lotto’ likiwa pia na takwimu za ligi tofauti za ndani ya nchi nz nje, na matangazo mbalimbali ya biashara.

 

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers maeneo ya Msasani na Kariakoo walizidi kumaga sifa kwa gazeti  hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kuwarahisishia masuala ya michezo ya kubeti.

 

 

Heshima ya Betika  imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia gazeti hilo kwa bei nafuu.

 

 

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Ili kufahamu namna ya kutangaza biashara zako, fika katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam ama kutembelea mitandao yetu ya kijamii ya Global Publishers.

 

(PICHA/HABARI NA DENIS MTIMA |GPL)

Leave A Reply