The House of Favourite Newspapers

Wafungwa 68 Wauawa Ecuador

0

MAMLAKA nchini Ecuador imesema kuwa wafungwa 68 wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa wakati wa makabiliano kati ya magenge ya uhalifu katika gereza la Guayas N1 la mji wa bandari wa Guayaquil katika Pwani ya Pasifiki.

 

Ofisi ya mwendesha mashtaka imesema kuwa idadi hiyo ya vifo ni kulingana na taarifa za awali na kuongeza kuwa imeanzisha uchunguzi kuhusu makabiliano hayo ya ghasia yalioanza siku ya Ijumaa usiku na kuendelea hadi jana asubuhi.

 

Hapo jana, idara ya kitaifa ya polisi imesema kuwa operesheni inaendelea katika gereza hilo la Guayas N1 kudumisha utulivu na uthabiti.

Leave A Reply