The House of Favourite Newspapers

Wahamiaji Haramu Waliovalia Sare za Vyama vya Siasa Wanaswa Moro

JESHI la Uhamiaji Mkoa Morogoro linawashikilia wahamiaji haramu 21 waliokamatwa maeneo mbalimbali huku baadhi yao wakidaiwa kutumia mabasi ya abiria, kuvaa jezi au sare za vyama vya siasa na mashuka ya kimasai ili wasigunduliwe kirahisi na kuingia nchini.

 

Naibu kamishna wa uhamiaji Mkoa wa Morogoro, Safina Muhindi amesema mbinu hiyo imebainika kutumiwa na wahamiaji hao haramu ili kujifanya kama wakazi wa maeneo ya kaskazini au mashabiki na wapenzi wa vyama vya siasa hali inayosababisha ugumu wa kuwabaini kirahisi na kuwakamata ambapo akawaasa wananchi kuwafichua kwani wamekuwa wakisabisha hasara kubwa kwa taifa na kutishia amani na usalama.

Muhindi amewaonya vikali wamiliki wa mabasi, madereva na makondakta kubeba ovyo abiria bila kujiridhisha na akabainisha sheria haitomuacha salama yeyote atakayehusika kuwasafirisha au kuwaingiza nchini wahamiaji hao na hapa anaonyesha baadhi ya madereva waliokamatwa kwa tuhuma hizo.

Comments are closed.