The House of Favourite Newspapers

WAHITIMU MAJENGO SEC. 2,000 WATOA MSADA VITUO VYA YATIMA

Mmoja wa wakilishi wa Kundi la WhatsApp la Wanafunzi wahitimu  mwaka 2,000  Sekondari ya Majengo  mkoani Kilimanjaro, Eng. Willbard Gandu (kulia) akikabidhi  msaada  kituo  cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa  wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo  Kilimanjaro, Eng, Maeda (kulia) akimkabidhi msaada.
Mmoja wa viongozi wa kundi hilo la wanafunzi waliohitimu Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto yatima ‘Green Pastures’, Mchungaji Douglas Kiseu sehemu ya msaada. 
Mhitimu 2,000, Oswald (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’  sehemu ya msaada.
Sehemu ya wawakilishi wa Kundi hilo mkoani mwanza wakipiga picha ya ukumbusho mara baadaa ya kukabidhi msaada katika kituo cha watoto yatima cha ‘Tanzania Childrens Rescue Centre (TCRC)’ jijini Mwanza.
Mmoja wa wahitimu Sekondari ya Majengo, Bi. Grace Minja (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto  yatima  msaada uliotolewa na wanafunzi hao.
Picha ya pamoja ya wawakilishi wa Dar es Salaam wa kundi la WhatsApp la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2,000 Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro.

 

KUNDI la WhatsApp la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2,000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro limetembelea vituo vitatu vya watoto wanaoishi katika maazingira maagumu na kutoa misaada mbalimbali ikiwa ni kuwafariji watoto hao.

 

 

Vituo vilivyonufaika na misaada hiyo ni pamoja na Kituo cha watoto yatima ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam, Kituo cha watoto yatima cha ‘Tanzania Childrens Rescue Centre (TCRC)’ jijini Mwanza na Kituo cha ‘Hope Village For Orphans and Vulnerable Children‘ cha mkoani Kilimanjaro.

 

Akizungumzia msaada huo mmoja wa viongozi wa kundi hilo la wanafunzi waliohitimu Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi alisema wanafunzi hao walichanga fedha kwa ajili ya kuwatembelea wahitaji ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 4 tangu kuanzishwa kwa kundi hilo.

 

 

“Wanakikundi waliamua kuchangishana fedha kwa ajili ya kuwatembelea wahitaji na kutoa chochote kwa lengo la kuwafariji yatima, na misaada kugawanywa katika mikoa mitatu yenye wawakilishi yaani Mwanza, Dar es Salaam na Mkoa wa Kilimanjaro…hii ni sehemu ya maadhimisho ya miaka minne ya kundi ambalo tulilianzisha 2014,” alisema Bw. Mushi.

 

 

Msaada uliyotolewa ni mifuko ya unga wa sembe, mchele, sukari, maharage, sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kupikia, madaftari, vyombo vya kutumia pamoja na peni.

 

 

Vingine ni pamoja na Dawa za meno, miswaki, biskuti, juisi, maji ya kunywa, mikate, majani ya chai, viatu pamoja na nguo mbalimbali za watoto vyote vikiwa na zaidi ya thamani ya zaidi ya milioni 1.8.

Comments are closed.