The House of Favourite Newspapers

Waimbaji wa Injili wamfuta machozi Cassian!

MSA­NII wa nyimbo za Injili nchini ambaye pia ni mlezi wa waimbaji wa injili Tanzania, Emmanuel Mbasha ameeleza jinsi yeye na waimbaji wen­zake walivyomfuta machozi msanii mwenzao Pascal Cassian ambaye alipata ajali ya gari siku za hivi karibuni.

MSHINDI BSS ALIA! “Niokoeni jamani, yaliyonikuta sitasahau”

Akizungumza na Ijumaa Wikienda Mbasha alisema kuwa, walichokifanya ni kuchangishana pesa na kumnunulia msanii huyo mahi­taji mbalimbali lakini kubwa ni kumpatia Bima ya Afya ili aweze kutibiwa kwa urahisi tatizo lake la kibofu cha mkojo alilonalo.

“Tuliguswa na hali yake ya kiafya tukaona tufanye kile kilicho ndani ya uw­ezo wetu, tumem­patia bima ya afya lakini pia tumempa vitu mbalimbali am­bavyo vitamsaidia katika kipindi hiki kigumu anachopitia,” alisema Mbasha.

STORI: Memorise Richard, Ijumaa Wikienda.

Part 2: MSHINDI BSS – “Madam Ritta Nakufa mimi nisaidie”

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.