The House of Favourite Newspapers

Wajapan wampiga stop Samatta… kumgusa Messi

0

samattaMbwana Samatta.

OSAKA, Japan
NDOTO ya nyota wa Kitanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kumkabili staa wa dunia, Lionel Messi wa Barcelona, zimeyeyuka baada ya jana Jumapili TP Mazembe kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Hiroshima ya Japan katika michuano ya Kombe la Dunia Ngazi ya Klabu inayoendelea nchini Japan.

Samatta ambaye ni mfungaji bora Afrika, alicheza dakika 90 katika mchezo huo hatua ya robo fainali, huku Ulimwengu akiingia dakika ya 46 akichukua nafasi ya Given Singuluma.

Iwapo TP ambao walikuwa wanaliwakilisha Bara la Afrika wangefuzu, wangekwaana na River Plate ya Argentina ambao ni mabingwa wa Amerika Kusini hatua ya nusu fainali na kama wangefanikiwa kuiondoa, basi nafasi ya kukutana na Barcelona fainali ilikuwa kubwa.

Barca wao wameanza hatua ya nusu fainali, wakitarajiwa kushuka dimbani Alhamisi wiki hii kupepetana na Guangzhou Evergrande ya nchini China iliyofuzu kwa kuichapa Club America ya Mexico.

Sasa TP itavaana na Club America katika mechi ya kutafuta mshindi wa tano itakayopigwa Jumatano ya keshokutwa.

Leave A Reply