The House of Favourite Newspapers

WAJUE WANAWAKE 12 WALIOANDIKA REKODI YA KUZAA WAKIWA VIKONGWE

 

Mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe na unaweza ukaolewa au ukawa na mwanaume lakini usipate mtoto kwa kipindi kirefu mpaka au ukaendelea kupata watot mpaka kwenye umri wa uzeeni.

 

Duniani wapo watu wengi ambao wamepata watoto katika miaka wasioitarajia lakini wamebidi tu waipokee huku wakiwa na machozi ya furaha.

 

Hawa ni baadhi ya wanawake 10 ambao wamefanikiwa kupata watoto wakiwa kwenye umri wa uzee kuanzia miaka 60 na kuendelea.

 

1.DALJINDER KAUR

 

Mwanamke huyu ni Raia wa India mwenye umri wa miaka 72 na mume wake ana umri wa miaka 75, wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume. Mwanamke huyu anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke mzee duniani kupata mtoto akiwa na umri wa miaka 72.

 

2. Rajo Devi Lohan

 

Mwanamke huyu pia ni raia wa India, amejifungua mtoto wake wa mwisho akiwa na umri wa miaka 69. Anashikilia rekodi ya mwanamama mzee ambaye stori yake haijawahi sajiliwa kabla. Repoti zinasema kwamba mtoto huyo ni mzima na mwenye afya tele.

 

3.Elizabeth Adeney

 

Ni mwanamke ambaye amefanikiwa kupata akiwa na umri wa miaka 66. Kwa ripoti zinasema mama yupo vizuri na mtoto akiendelea katika hali salama na mwenye afya. Elizabeth kwa wakati huu amekuwa akipata fursa za kuwa kwenye vipindi vya redio na televisheni.

 

4.Bhateri Devi Singh

 

Mwanamke raia wa India na amefanikiwa kupata watoto mapacha watatu akiwa na umri wa miaka 66. Watoto hao wanakuwa vizuri huku mama yao akiwa katika hali nzuri.

 

5.Adriana Iliescu

 

Mwanamke raia wa Romania alisubiri kupata watoto mapacha watatu akiwa na umri wa miaka 66 lakini alifanikiwa kumpata mmoja aliyefanikiwa kuishi baada ya kujifungua. Mtoto kwa wakati huu ni moja kati ya watoto wanaopendwa na watu wa Roman karibia wote .

 

6.Omkari Panwari

 

Mwanamke raia wa India alifanikiwa kupata watoto wawili mapacha wakike na wakiume akiwa na umri wa miaka 67 baada ya kufanyiwa matibabu lakini baadaye alifariki dunia kutokana na matatizo ya kiafya.

 

7.Maria Del Carmen Bousada De Lara

 

Mwanamke raia wa Hispania na alifanikiwa kupata watoto mapacha wawili akiwa na miaka 66. Ripoti zinasema kwamba mara ya kwanza alimdanganya daktari kwamba ana umri wa miaka 55. Mwanamke huyo alifariki miaka miwili baada ya kujifungua.

 

8.Valentyna Pidverbana

 

Mwanamke raia wa Ukraine alifanikiwa kupata mtoto wa kwanza na pekee akiwa na miaka 66. Bado anaishi mpaka wakati huu huku akiwa na afya ya kuridhisha.

 

9. Annegret Raunigk

 

Mwanamke raia wa Ujerumani na alifanikiwa kupata watoto mapacha wanne huku akiwa na umri wa miaka 65.Kwa ujumla ana watoto 17  ambapo alikomea akiwa na umri wa miaka 44 kabla ya kujifungua hao mapacha. Ni mwanamke mzee anayeshikilia rekodi huko Uropeani kwa kuwa na watoto na kujifungulia kwenye umri wa miaka ya 60.

 

10.Memnune Tiryaki

 

Raia wa India ambaye amefanikiwa kupata mtoto wa kwanza akiwa na umri wa miaka 62.

 

11.Dawn Brooke

 

Mwanamke raia wa Uingereza na alifanikiwa kupata mtoto wa kwanza akiwa na umri wa miaka 59. Amesajiliwa kwenye kitabu cha rekodi cha Guiness cha dunia kuwa mwanamke mzee zaidi kupata mtoto kwa umri huo.

 

12.Raisa Akhmadeeva

 

Mwanamke raia wa Urusi na alifanikiwa kujifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 56.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Utukufu wa Mungu Unavyoimarisha Uhusiano wa Tanzania, Kenya!

Comments are closed.