The House of Favourite Newspapers

Wakala Mkubwa wa Wanamichezo Duniani, Sal Jobe Kutua Bongo Kusaka Vipaji

0
Sal Jobe akiwa na mmoja kati ya mabondia aliosimamia uhamisho wao

 

WAKALA mkubwa wa wanamichezo mbalimbali wakiwemo wanasoka na mabondia, Sal Jobe anatarajiwa kutua nchini Tanzania wakati wa maandalizi ya msimu mpya, kabla ya dirisha la uhamisho la kimataifa kufungwa ambapo anatarajiwa kukutana na vijana wenye vipaji mbalimbali kwa ajili ya kuwatafutia masoko Ulaya.

 

Sal Jobe ambaye awali alikuwa mwigizaji kabla ya kubadilisha kazi na kuwa wakala wa wanamichezo, amesema anajisikia furaha kuwa na mipango ya kuja Tanzania na anaamini atawapata vijana wengi wenye vipaji mbalimbali na kuwasaidia kwenda kutimiza ndoto zao barani Ulaya.

 

Jobe ambaye mpaka sasa ameshafanikiwa kuwasafirisha wanamichezo zaidi ya 30 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na kuwapeleka Ulaya, amesema atakuja nchini ndani ya mwezi Agosti.

 

“Kwa marafiki zangu wote nchini Tanzania, nawahakikishia kwamba nitakuja huko mwezi Agosti kutafuta vijana wenye vipaji,” alisema.

 

Jobe ambaye pia ni mwandishi wa Kitabu cha Mchezo wa Wakala, amepata umaarufu katika biashara ya wanamichezo, ambapo ameshiriki kufanikisha ‘deals’ za uhamisho wa wanasoka na mabondia maarufu kwenda barani Ulaya.

 

Leave A Reply