Katika kusherehekea Sikukuu ya Wapendanao, maafisa kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania jana walitoa zawadi kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Global Group inayozalisha Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Amani, Risasi, Ijumaa Wikienda, Championi, Spoti Xtra pamoja na kumiliki Global TV Online.
Zawadi hiyo ambayo ni dumu la lita tano la asali halisi ilikabidhiwa na Meneja Mawasiliano wa taasisi hiyo, Glory Mziray na afisa habari wake, Tulizo Kilaga kwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Abdallah Mrisho.
Akizungumzia zawadi hiyo, Glory alisema kuwa, wameamua kuitoa ikiwa ni kuonesha upendo wao kwa wafanyakazi wa Global na kuimarisha ushirikiano mwema na vyombo mbalimbali vya habari nchini.
“Tumefanya hivi kwa vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni katika jitihada zetu za kujenga ushirikiano mwema, tunajua umuhimu wenu katika sekta ya misitu hivyo tunaamini tutazidi kushirikiana katika mambo mbalimbali.
“Lakini pia tupo kwenye msimu wa wapendanao, tunawapenda na ndiyo maana tumeamua kuwaletea zawadi hii,” alisema Glory.
PICHA NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS
Comments are closed.