KAMPUNI ya Liqui Moly imeingiza bidhaa mpya za oili na vilainishi vya magari na mitambo kutoka nchini Ujerumani.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Liqui Moly, Faraja Mkinga, alisema kampuni yake ina fahari kubwa kuwapatia Watanzania bidhaa zenye ubora wakati taifa likijipanga kuelekea katika uchumi wa kati.
“Bidhaa zetu ni za ubora wa hali ya juu, zinapatikana katika bei inayoendana na hali ya uchumi. Zipo za aina tofauti kama vilainishi vya magari madogo, magari ya usafirishaji, meli, majenereta, pikipiki na hata ndege.
Ameongeza kuwa kwa sasa bidhaa hizo zinapatikana jijini Dar es Salaam kwenye ofisi zilizopo Mikocheni B na mawakala mbalimbali na kwamba humsaidia mteja kupunguza gharama za uendeshaji wa magari na mitambo.
“Kampuni imeingiza oili itakayomwezesha mdau kutumia chombo chake hadi kilomita 15,000 tofauti na oili nyingine hapa nchini zinazoenda kilomita 3,000 mpaka 9,000 tu.
Comments are closed.